Thursday, April 9, 2015
WAZIRI STEVEN WASSIRA AWAFUKUZA KAZI WATU KWA MATMUMIZI MABAYA YA OFISI.
Do you like this story?
WAZIRI wa kilimo,
Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi wakurugenzi watendaji watatu
wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin
Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma
ambayo yameitia hasara ya Bilioni 2.5 Serikali .
Akitoa agizo hilo leo
mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira amewataja Watendaji hao kuwa ni
Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi
wa Mipango na Uwekezaji; na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala.
Wassira amesema
baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijiji vya
Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa shirika hilo, aliunda timu
ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko
hayo.
“Baada ya kuunda
tume kutoka hapa Wizarani ikishirkiana na Hazina,
walienda kwenye shirika hilo kufanya ukaguzi.Tume ilibaini
kwamba mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi hawa
walijifanya wahasibu, wakawa wanakuanya pesa
wenyewe na kutembea nazo.Walifanya maksudi tu ili
kujiwekea mianya ya kuiba Fedha”Amesema Wassira
Taarifa ya Mheshimiwa
Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748 billion zilizokuwa zimekusanywa
kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606 milioni tu ndizo zimetumika kihalali
wakati kiasi kilichobaki kimetumika bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha
za umma.
Waziri Wassira
amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini kwamba watendaji hao
wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi yaliyo kinyume
cha utaratibu
ikiwemo pesa
zilizotengwa kwa ajili maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo
zimetumika ndivyo sivyo.
Vilevile Waziri Wassira
amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa ajili ya kupelekwa kwenye
mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa na watendaji , tena kwa makusudi
pasipo kupelekwa huko.
Aidha,Waziri Wasira
amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya shirika la Ludaba
kuwafukuza kazi mara moja watendaji hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja
huku taratibu na sheria za kuwafikisha mahakamani zikifanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI STEVEN WASSIRA AWAFUKUZA KAZI WATU KWA MATMUMIZI MABAYA YA OFISI.”
Post a Comment