Thursday, April 9, 2015
UMEME KUNUFAISHA VIJIJI 93 NJOMBE NA IRINGA
Do you like this story?
WATEJA wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mikoa ya Iringa na Njombe wanatarajia
kuongezeka kutoka 63,300 wa sasa hadi zaidi ya 93,000 ifikapo mwaka 2017.
Ongezeko hilo
linakwenda sambamba na kuviunganisha vijiji vipya 93 baada ya vingine 84 katika
mikoa hiyo kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa kupitia awamu ya pili ya mradi
wa usambazaji umeme vijijini unaotekelezwa kupitia Wakala wa Umeme Vijijini
(REA).
Meneja wa
Tanesco mkoani Iringa, Sarah Assey akizungumza ofisini kwake jana alisema
ongezeko hilo la wateja 30,000 wapya kwa mpango wa kuwaunganisha 15,000 kila
mwaka, litakwenda sambamba na matumizi ya mita za Luku kwa wateja wake wote.
“Mpango wa
shirika ni kuona wateja wetu wote wanafungiwa mita za Luku ifikapo mwaka 2017;
mpango utakaohitimisha matumizi ya mita za zamani,” alisema na kuongeza kwamba
mpaka sasa zaidi ya wateja 38,000 katika mikoa hiyo wamekwishafungiwa mita za
Luku.
Alisema mpango
wa kuwaunganisha na mita za Luku wateja wao wote utapunguza ajira ya wasoma
mita na hivyo kupunguza matumizi ya shirika.
Alisema Tanesco
inataka kuondokana na matumizi ya mita za zamani kwa wateja wake kwa sababu
ufanisi wake unazidi kushuka hivyo kulisababishia hasara.
Meneja huyo
alisema kuachana na matumizi ya mita hizo za zamani kutamaliza pia kile
kinachoonekana kama kero wanayopata wateja wao wakati wa kulipia Ankara zao
katika ofisi za shirika hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UMEME KUNUFAISHA VIJIJI 93 NJOMBE NA IRINGA ”
Post a Comment