Thursday, April 9, 2015

FACEBOOK YAZINDUA TOVUTI YA MESSENGER.


Muonekano wa tovuti ya Messenger katika kompyuta na simu.



UNAKUMBUKA mtandao wa Facebook ulipowalazimisha watumiaji wake kupakua (download) huduma ya Messenger kwa ajili ya simu za mkononi mwaka jana? Sasa Facebook imezindua tovuti ya huduma yake ya Messenger ambayo ni www.messenger.com.

Tovuti hiyo itakuwa na kiwambo kwa kikubwa (full-screen) itakayoonyesha mawasiliano ya watumiaji na itamwezesha mtumiaji kuweka dondoo (notifications) mbalimbali na kuweza kuzima kwa muda mawasiliano.

Kama ilivyokuwa awali katika huduma ya Messenger kwenye Facebook.com, mtumiaji ataweza kutuma picha, stika kwa watu wake kupitia Messenger.com
Unapoingia katika tovuti hiyo kwa kutumia taarifa zako za Facebook, Messenger.com inakusanya meseji zako za karibuni na inazionyesha katika kiwambo kwa ukubwa (full-screen).

Hapo mtumiaji ataweza kupiga simu au kuchati kwa kutumia video (video chats) kupitia menyu zilizopo juu mkono wa kulia na kwa upande wa kushoto mtumiaji ataweza kupunguza au kuongeza sauti, kuona dondoo mbalimbali na kuweza kumzuia mtumiaji mwingine.

Messenger.com kwa sasa inapatikana kwa lugha ya Kiingereza, ila Facebook itaongeza huduma ya lugha nyingine karibuni. Mbali na hilo, tovuti mama ya Facebook itaendelea kuwa na huduma yake ya Messenger kama zamani.

Huduma ya Facebook Messenger inatumiwa na watu zaidi ya milioni 600 kwa mwezi. Kwa ujumla mtandao wa Facebook unatembelewa na takribani watu bilioni 1.4 kwa mwezi huku watu takribani milioni 890 wakitembelea Facebook na kutazama zaidi ya video bilioni tatu kwa siku.

Mwaka uliopita, Facebook walinunua mtandao wa WhatsApp kwa Dola za Kimarekani bilioni 19. Mwaka huu WhatsApp walizindua huduma yao kupitia kwenye kompyuta ambayo inamuonekano kama wa Messenger.com.

Kwa sasa WhatsApp inayo huduma ya kupiga simu kupitia simu za Android na katika wiki za karibuni itazindua huduma hiyo katika simu zinazotumia iOS.

0 Responses to “FACEBOOK YAZINDUA TOVUTI YA MESSENGER.”

Post a Comment

More to Read