Thursday, April 9, 2015

MTANZANIA ALIYEKAMATWA KWA SHAMBULIO LA GARRISA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO.




Mtanzania aliyekamatwa Kenya akishukiwa kuhusika na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliyopita lililosababisha vifo vya watu takribani 150 na wengine wengi kuachwa majeruhi, Rashid Charles Mberesero mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma, lakini uongozi wa shule hiyo umesema kuwa, Rashid alitoweka shuleni hapo tangu Desemba mwaka jana.
Habari zilizothibitishwa na wazazi wake ni kwamba mwanafunzi huyo anasoma katika Shule ya Sekondari ya Bihawana, Dodoma, baada ya kufaulu katika Shule ya Sekondari Gonja mkoani Kilimanjaro.

Taarifa hizo zimekuja wakati Mberesero maarufu kwa jina la Rehani Dida, akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo jijini Nairobi baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani juzi.
CHANZO: ITV TANZANIA

0 Responses to “MTANZANIA ALIYEKAMATWA KWA SHAMBULIO LA GARRISA KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO.”

Post a Comment

More to Read