Thursday, April 9, 2015
MFUMUKO WA BEI WATAIFA WAONGEZEKA.
Do you like this story?
Na Veronica Kazimoto, Takwimu
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi 2015 umeongezeka kidogo
hadi kufikia asilimia 4.3 ikilinganishwa na asilimia 4.2 za mwezi Februari
kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali
nchini.
Akitoa taarifa ya mfumuko huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa
Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo
amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na badiliko la bei ya bidhaa na huduma
kati ya mwezi Machi na Februari 2015.
Amesema bei ya vinywaji baridi na bidhaa za vyakula ikiwemo Mchele,
Ungawa Muhogo, nyama, Samaki, Maharage, Choroko na Sukari kwa mwezi Machi
imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Februari.
Amesema Mfumuko wa Bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa
asilimia 0.7 mwezi Machi ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.6 za mwezi
Februari huku Fahirisi za bei kwa mwezi Machi zikiongezeka hadi 155.88 kutoka
154.83 za mwezi Februari, 2015 kutokana na ongezeko la bei ya mchele, Samaki,
matunda aina ya machungwa, maharage, mboga mboga na sukari.
Aidha, amefafanua kuwa kiwango cha Mfumuko wa bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Machi 2015
kimeongezeka hadi kufikia asilimia 5.9 ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwezi
Februari 2015.
Akitoa ufafanuzi kuhusu uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua
bidhaa na huduma kwa mwezi Machi 2015 amesema kuwa umepungua na kufikia
shilingi 64 na senti 15 ikilinganishwa na shilingi 64.59 za mwezi Februari
2015.
Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi kwa baadhi ya nchi za Afrika
Mashariki amesema una mwelekeo unaofanana Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei wa
asilimia 1.90 kutika asilimia 1.4 za mwezi Februari huku Mfumuko wa Bei
nchini Kenya kwa mwezi Machi 2015 ukiongezeka hadi kufikia asilimia 6.31 kutoka
asilimia 5.61 za Februari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFUMUKO WA BEI WATAIFA WAONGEZEKA.”
Post a Comment