Thursday, April 9, 2015
ALICHOKISEMA 'BIG BOSI' MWAMBUSI BAADA YA SARE NA AZAM FC.
Do you like this story?
MCHEZO wa ligi
kuu ya soka Tanzania bara kati ya Azam Fc na City uliopigwa jana Chamanzi
Complex Mbagala jijini Dar umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo
uliokuwa mzuri na wakuvutia Azam walikuwa wa kwanza kuleta kashkash
kwenye lango la City baada kipre Balou kupiga mpira mrefu uliotuwa sawia
kwenye kichwa cha John Bocco lakini uimara wa kipa Hannington Kalyesubula
aliwafanya wenyeji hao kushindwa kupachika bao.
Dakika kumi baadae
City ilijibu mashabulizi kupitia Paul Nonga aliyefanikiwa kumtoka mlinzi
Pascal Wawa lakini mpira alioupiga ulishindwa kulenga lango, timu
ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hadi dakika 45 za kwanza
zinakamilika hakuna timu iliyofanikiwa kufunga bao.
Azam walikianza
kipindi cha pili kwa nguvu hasa kufuatia mabadiliko ya kumtoa John Bocco na
kuingia Amri kiemba ambapo dakika ya 61 kipre Balou alifanikiwa kukokota mpira
kutoka katikati uwanja na kupiga shuti lilikwenda moja kwa moja wavuni
kuiandikia timu yake bao la kuongoza.
Hata hivyo bao hilo
halikudumu kwani dakika nne tu baada ya kungia City ilifanikiwa kusawazisha kwa
mkwaju wa penalti iliyopigwa na Rafael Daud Alfa baada ya Deus Kaseke
kuangushwa kwenye eneo la hatari wakati akijiandaa kupachika bao.
City ilifanya
mabadiliko kwa kuwatoa Deus Kaseke na Paul Nonga na nafasi zao kuchukuliwa na
Peter Mapunda na Hamad Kibopile mabadiliko ambayo yaliisaidia kuongeza
nguvu ya mashambulizi langoni mwa Azam lakini mpaka dakika 90
zinamalizika matokeo yalibaki 1-1.
Kocha wa City Juma
Mwambusi amewashukuru wachezaji kwa kupambana na kufanikiwa kupata pointi moja
kwenye mchezo huo huku akiwataka kujiandaa kwa vita nyingine ya mchezo wa ligi
dhidi ya Yanga jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa.
“Nashukuru mmepambana,
tumepata pointi moja ni jambo zuri kwetu kwa sababu tutakuwa tumesogea
kwenye nafasi nyingine, tuna mchezo jumapili hivyo tujiandae na
tujue kuwa tunatakiwa kuipigania timu yetu mpaka dakika ya mwisho”
alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ALICHOKISEMA 'BIG BOSI' MWAMBUSI BAADA YA SARE NA AZAM FC.”
Post a Comment