Thursday, April 9, 2015

ZITO KABWE AIGEUKA FRIENDS OF SIMBA.




Mjumbe wa zamani wa Kamati ya Fedha ya klabu hiyo, Zitto Kabwe amefichua kinachoiua Simba kwa sasa akisema kwamba viongozi wa timu hiyo hawatakiwi kufanya kazi peke yao.

Zitto alisema Simba haiwezi kufanikiwa kama itaendelea kuwa na makundi na kusababisha kutokuwa na umoja na mshikamano kwa wanachama wote.

Alisema Simba haiwezi kuongozwa na wanachama wa Friends Of Simba pekee bali ni lazima ijumuishe wanachama wengine ili kuchangia maendeleo ya timu yao kwa namna moja au nyingine.

Mwanasiasa huyo machachari alisema kinachoiua Simba kwa sasa ni makundi ambayo viongozi wa wameshindwa kuyadhibiti.

“Kama kuna vitu vinaweza kudumaza maendeleo katika sekta yoyote ile basi ni makundi, hivyo lazima viongozi wa Simba waepuke kuwa upande mmoja kama inavyoonekana Friends of Simba ndio wana makali kuliko wengine,” alisema Zitto aliyekuwa mjumbe enzi za uongozi wa Ismail Aden Rage.
Pia alisema kutokana na mwenendo huo, Simba inakatisha tamaa hata mashabiki wao.

“Simba ya sasa si ile ya miaka iliyopita inafungwa ovyo na timu zilizotakiwa zijifunze kitu kutoka kwao, lazima viongozi wakae chini na wakubali kuondoa makundi ili walete mabadiliko,” alisema.

Alisema kitendo cha Simba kuongeza chipukizi timu ya taifa ni uthibitisho kuwa timu yao ni bora na inapaswa kuwa mfano.

“Lazima viongozi wawe na uamuzi mgumu vinginevyo Simba itazidi kuporomoka,’’ alisema.
Source: Mwanaspoti

0 Responses to “ZITO KABWE AIGEUKA FRIENDS OF SIMBA.”

Post a Comment

More to Read