Friday, April 10, 2015
MGOMO WA MADEREVA WATIKISA DAR.
Do you like this story?
MADEREVA wa mabasi ya mikoani
na daladala wa jijini Dar leo wamefanya mgomo kupinga agizo la Mamlaka ya
Kudhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) lililowataka kwenda kusoma
katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Mwandishi wetu amezunguka maeneo
tofautitofauti jijini Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani
pamoja na daladala za maeneo tofauti ya Jiji la Dar.
Mwandishi wetu pia aliweza kufika eneo la
Stendi ya Ubongo na kujionea hali ilivyokuwa asubuhi na kuzungumza na baadhi ya
madereva ambao walikuwa na kauli tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.
Mmoja wa madereva ambaye alijitambulisha kwa
jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya kazi zake kati ya Dar es Salaam na
Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya kutokufanya shughuli zake ni kutokana na
kikao ambacho walipanga kukifanya leo kujadili agizo la Sumatra lililowataka
waende shule kusoma.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina
moja la Khamis anayefanya shughuli zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema
sababu iliyomfanya agome ni kupinga sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na
jeshi la polisi kuwataka madereva wote wa abiria (Pasangers Services Vehicle)
kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa gharama ya shilingi laki tano.
Khamisi alisema sheria hiyo inawabana sana
madereva kwani moja kati ya vipengele vya sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva
yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi hakuna faini yoyote bali
unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kumaliza siku hizo,
anapelekwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
“Hii sheria inatubana sana, mtu ukihitaji
kubadilisha leseni yako ikipitwa na muda unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma
darasani kwa muda wa wiki mbili kwa ada isiyopungua laki tano na kuendelea kitu
ambacho kinatuumiza sisi madereva,” alisema Khamis.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGOMO WA MADEREVA WATIKISA DAR.”
Post a Comment