Tuesday, April 14, 2015
WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOTEKWA NIGERIA WAKUMBUKWA BAADA YA MWAKA 1
Do you like this story?
Wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na Boko Haram mwaka jana. |
MAADHIMISHO
ya mwaka mmoja tangu wasichana zaidi ya 200 kutekwa na Kundi la Boko Haram huko
Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria yanafanyika leo Nigeria.
Wasichana zaidi ya 200 walitekwa Aprili 14,
mwaka jana na kuitikisa dunia huku baadhi ya mataifa kama Marekani na China
yakiahidi kusaidia upatikanaji wa wadada hao japo mpaka sasa bado
hawajapatikana.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika Mji Mkuu
wa Nigeria, Abuja huku wasichana 219 wakiwepo kuwakilisha wale waliopotea.
Maadhimisho hayo pia yatafanyika sehemu
nyingine kama London na Washington.
Jana Jumanne, Shirika la Amnesty
International lilieleza kuwa wasichana na wanawake 2,000 wametekwa na Kundi la
Boko Haram tangu kuanza kwa mwaka jana huku wakifanywa wapishi, watumwa wa
ngono na wapiganaji.
Upoteaji wa wasichana hao ulipelekea kampeni
ya #BringBackOurGirls iliyoenea katika mtandao wa Twitter huku ikiungwa mkono
na watu mashuhuri duniani akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama na
mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WASICHANA ZAIDI YA 200 WALIOTEKWA NIGERIA WAKUMBUKWA BAADA YA MWAKA 1”
Post a Comment