Friday, May 15, 2015
MKAPA AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI.
Do you like this story?
RAis mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam. |
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali. Picha/Aron Msigwa -MAELEZO. |
Na Aron Msigwa,MAELEZO .
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin
Mkapa amewataka Wakandarasi kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi na
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi
wanayoisimamia na kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.
Mhe.Mkapa ameyasema hayo leo jijini Dar es
Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi
(CRB) uliowawajumuisha pia wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na
Kenya.
Amesema umakini katika usimamizi wa kazi za
wakandarasi na uwepo wa wataalam waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia
kwa kiasi kikubwa kasi maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.
Ameeleza kuwa sekta ya ujenzi ndiyo
iliyolifikisha taifa hapa kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa
unaofikia asilimia 14.1 ikifuatiwa na sekta nyingine na kuongeza kuwa ili nchi
iweze kuendelea lazima wakandarasi wazalendo wajengewe uwezo ili kuhakikisha
kuwa fedha zinazotolewa katika sekta ya ujenzi zinabakia Tanzania na
kuwanufaisha wazawa badala ya wageni.(Muro)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKAPA AWATAKA WAKANDARASI NCHINI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI. ”
Post a Comment