Tuesday, June 30, 2015

TIMU ZITAKAZOTUMIA MAKOCHA WASIO NA LESEN B KUFUTWA LIGI KUU


Rais wa TFF, Jamal Malinzi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu swala la makocha jijini mbeya.




(Picha na David Nyembe wa Fahari News)




SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limezichimba mkwara klabu za Ligi Kuu zitakazoendeleza utamaduni uliozoelekwa wa kuajiri makocha wasio na utaalamu wala cheti cha ngazi B cha CAF kuwa,  hazitaruhusiwa kushiriki ligi kuu msimu huu,  unaotarajiwa kuanza miezi miwili ijayo.

Kadhalika, TFF imesisitiza kuwa, Klabu zitakazoshindwa kutimiza masharti ya mfumo mpya wa kushiriki ligi hiyo ya kuwa na leseni ya uendeshaji wa klabu kwa kuwa na uwanja wa mazoezi, uwanja wa kuchezea mechi na programu ya vijana, zikiwemo timu za Azam na Yanga hazitoruhusiwa kushiriki michezo ya kimataifa.

Tamko hilo limetolewa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, wakati akielezea programu ya mazoezi na maandalizi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) mkoani hapa.

Timu hiyo inanolewa na kocha Bakari Shime, ipo kwenye programu maalum ya TFF ili kuhakikisha Tanzania inakua na kikosi bora cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

Akizungumzia suala hilo la timu za Ligi Kuu kutumia makocha wenye leseni B, Malinzi alisema kuwa kigezo hicho kinalenga kuboresha mchezo wa soka hapa nchini.


Aidha, Malinzi alisema kuwa vigezo hivyo haviishi kwa makocha wakuu pekee bali hata kwa makocha wasaidizi nao watatakiwa kuwa na leseni daraja C  ili waweze kuwa wasaidi katika timu za Ligi Kuu.

Kuhusu suala la klabu za Ligi Kuu Bara kutumia mfumo mpya wa kushiriki ligi hiyo kwa kujaza fomu za kuomba ushiriki endapo itakidhi vigezo ikiwamo kuwa na uwanja wa mazoezi, uwanja wa kuchezea mechi na programu ya vijana.

Alisema halina mjadara katika mukhtadha wa soka la kisasa na maendeleo yake, hivyo vilabu vinapaswa kuelewa suala hilo kabla ya kujikuta zikikosa kushiriki ligi kuu.




0 Responses to “TIMU ZITAKAZOTUMIA MAKOCHA WASIO NA LESEN B KUFUTWA LIGI KUU”

Post a Comment

More to Read