Tuesday, June 30, 2015
WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA ZA ARDHI.
Do you like this story?
MTANDAO
wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanayojishughulisha na masuala ya
kilimo endelevu – PELUM Tanzania imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
kuhusu sera na sheria za ardhi.
Akizungumza
katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika mjini Morogoro mratibu wa PELUM
- Tanzania DONATI SENZIA amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kutokana na
changamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo za migogoro ya ardhi inayoendelea
hapa nchini.
PELUM–Tanzania
imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitatu ya Dodoma,
Iringa na Morogoro yanayohusu masuala ya ardhi , sera na sheria ili kuwajenga
uwezo katika kuripoti stori hususani habari za migogoro ya ardhi.
Mada
zilizotolewa katika mafunzo haya ni sera na sheria za ardhi namba 4 na namba 5
ya mwaka 1999, haki za kumiliki ardhi na maadili ya uandishi wa habari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA ZA ARDHI.”
Post a Comment