Tuesday, June 30, 2015

WAUZAJI WA MAFUATA WANAOYAFICHA ILI WAYAUZE KUANZIA TAREHE 01.07 KUKIONA CHA MOTO




Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji - EWURA imewataka wamiliki wote wa matanki ya kuhifadhia mafuta pamoja vituo vya mafuta kutothubutu kuhodhi mafuta kwa nia ya kuyauza baadaye katika kipindi hiki kuelekea kuanza kwa utekelezaji wa bajeti mpya ya mwaka 2015/2016 ambayo inatarajiwa kuanza kutumika julai mosi mwaka huu.

**Kauli hiyo imetolewa na afisa mkaguzi mkuu wa petroli - EWURA Suleiman Shaban walipotembelea baadhi ya maghala ya mafuta ili kujiridhisha endapo nishati hiyo inaendelea kusambazwa kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuwa hakuna huduma katika baadhi ya vituo vya mafuta.

Meneja uhusiano na mawasiliano Ewura Titus Kaguo amewatoa hofu wananchi kufuatia ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa nishati hiyo haitapatikana kwa siku ya jumatatu na jumanne hivyo wanunue mafuta ya kutosha ambapo amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote..

Hata hivyo kwa mujibu wa Ewura bidhaa hiyo yaweza kupanda katika ya sh.2300 hadi 250 kwa lita kufuatia ongezeko la tozo katika nishati hiyo iliyopitishwa na bunge lakini pia kupanda kwa dola na kushuka kwa thamani ya shilingi.

0 Responses to “WAUZAJI WA MAFUATA WANAOYAFICHA ILI WAYAUZE KUANZIA TAREHE 01.07 KUKIONA CHA MOTO ”

Post a Comment

More to Read