Tuesday, June 30, 2015

WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE ATOA MAAGIZO KUHUSU UINGIZAJI WA MAFUTA.




Waziri Nishati na madini George  Simbachawene amewataka maofisa wa serikali kusimamia kwa makini uingizaji mafuta katika Bohari za tanga ili kuepusha udanganyifu na kuruhusu kuingiza mafuta ambayo hayapo katika viwango vya ubora nchini na kuliletea taifa hasara.

Agizo hilo amelitoa wakati  akikagua miundombinu iliyojengwa na makampuni mbalimbali kabla ya kuanza kwa zoezi  la upakuaji wa shehena ya mafuta katika bandari ya Tanga.

Amesema kuwa uingizaji wa shehena ya mafuta katika bandari ya Tanga utapunguza msongamano  katika bandari ya Dar es salaam na kuongeza fursa za kiuchumi  kwa mkoa wa tanga

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usambazaji mafuta GBP Badar Masoud ameupongeza uwamuzi wa serikali wa kuitumia bandarai ya Tanga kwa ajili ya kupakulia mafuta na kuesema kuwa  utapunguza gharama za upakuaji wa mafuta tofauti na hapo awali.

Uingizaji wa mafuta katika bandari ya tanga utaanza julai 4 mwaka huu baada ya serikali kusimamisha zoezi hilo kwa zaidi ya miaka sita

0 Responses to “WAZIRI GEORGE SIMBACHAWENE ATOA MAAGIZO KUHUSU UINGIZAJI WA MAFUTA.”

Post a Comment

More to Read