Tuesday, June 30, 2015

WAMACHINGA WAPINGA MANISPAA YA ILALA KUWAPANGIA RATIBA YA KUFANYA BIASHARA.




Manispaa ya ilala imeweka mpango wa majaribio wa miezi mitatu kwa kutenga maeneo maalum ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga katika jiji la dar es salaam.

Maeneo yaliyotegwa ni mtaa wa kongo, nyamwezi, swahili, sikukuu, narungombe, tandamiti, pembe, mchikichi, pamoja na mahiwa.

Akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa jiji la DSM, mkurugenzi wa manispaa ya ilala isaya mngurumi amesema mpango huo wa majaribio umetokana na vikao vya manispaa hiyo pamoja na wadau mbalimbali vya kuoana namna ya ya kuweka mfumo bora utakaosaidia wamachinga kufanya biashara zao bila usumbufu.

Hata hivyo wafanyabiashara hao wamekataa kuafiki muda waliowekwa katika  mpango huo wa kutengewa maeneo maalum ya biashara ambapo kwa mujibu wa manispaa ya ilala wanatakiwa kufanya biashara kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa kumi kamili jioni mpaka saa tatu usiku na jumamos saa saba mchana hadi saa tatu usiku huku jumapili ni saa 1 asubuhi hadi saa tatu usiku

0 Responses to “WAMACHINGA WAPINGA MANISPAA YA ILALA KUWAPANGIA RATIBA YA KUFANYA BIASHARA.”

Post a Comment

More to Read