Thursday, July 2, 2015

BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA UPINZANI KUGOMEA MISWADA




BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirishwa ghafla leo baada ya wabunge wa upinzani kusimama na kukataa kutoka nje ili kuzuia miswada mitatu muhimu ya Gesi, Petroli na Uziduaji kusomwa kwa Hati ya Dharura.

Hali hiyo imetokea baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika kuomba mwongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge kwa kuwekwa miswada mitatu sambamba.
Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwataka wabunge hao kutoka nje kama hawataki kuendelea na kikao ila baada ya kugoma kufanya hivyo na kusimama kisha kuanza kupiga kelele, Spika aliamua kuahirisha bunge.
Miswada iliyowasilishwa ni hii hapa:

1.Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015)
2.Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015)
3.Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015

0 Responses to “ BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA UPINZANI KUGOMEA MISWADA”

Post a Comment

More to Read