Thursday, July 2, 2015
TFF YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA MWAKELEBELA, MWAMBUSI
Do you like this story?
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine
ametuma salamu za rambi rambi kwa famili aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa
TFF, Fredrick Mwakalebela kufuatia kufiwa na baba yake mzazi jana mjini
Irinnga na mazishi yakitarajiwa kufanyika kesho mjini Iringa.
Aidha
TFF imetuma salam za rambi rambi kwa kocha mkuu wa timu ya Mbeya City,
Juma Mwambusi kufutia kufiwa na mama yake mzazi mjini Mbeya.
TFF
pia imetuma salam za rambi rambi kwa familia ya mtangazi maarufu wa wa
michezo nchini Ezekiel Malongo aliyefariki dunia jana.
Katika
salam zake kwa familia ya Mwakalebela, Mwambusi na Malongo, Mwesigwa
amesema wanawapa sana pole wafiwa kwa kuondokewa na wapendwa wao na
kusema kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania wote wapo nao
pamoja katika kipindi hichi cha maombolezo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA MWAKELEBELA, MWAMBUSI ”
Post a Comment