Thursday, July 2, 2015
MWANACHAMA SIMBA AKIFIWA KULIPWA 250,000/
Do you like this story?
KLABU ya Simba imefanya kweli tena baada ya
leo kuzindua kadi mpya za uanachama ambazo zitatoa fursa kwa watakaojiunga
kunufaika na bima ya maisha.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kadi
hizo jijini Dar es Salaam leo mchana, Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, amesema
kila mwanachama atakayejiunga na kuchukua kadi mpya, atapata bima ya maisha
inayojulikana kwa jina la 'Simba Pamoja'.
Amesema bima hiyo itampatia mwanachama ambaye
amelipa malipo yake ya mwaka ya uanachama fedha taslimu zisizopungua Sh. 250,000
ikiwa atapata msiba kwa kufiwa na mtoto, mke ay yeye mwenyewe.
Aveva amesema malipo ya uanachama
hayajabadilika na yanaendelea kuwa Sh. 1,000 kwa mwezi, hivyo mwanachama
atalipa ada ya mwaka Sh. 12,000 kwa wanachama hai na Sh. 30,000 kwa wanachama
wapya.
“Hii ndiyo klabu pekee Afrika Mashariki na
Kati inayotoa fao hili kwa wanachama wake, Simba inajali sana wanachama wake na
tutaendelea kuimarisha uhusiano wa klabu na wanachama,” amesema Aveva.
Aveva ambaye alikuwa amefuatana na makamu
wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya
EAG Group, Imani Kajula, pia amezindua kadi ya Simba kwa ajili ya watoto
wanaoipenda timu hiyo 'Simba Cub Membership Card' ili kuwawezesha kutambuliwa
na kuwa wanachama wa timu hiyo.
“Kadi ya Simba Cubs itawawezesha watoto siyo
tu kutambuliwa kuwa wanachama wa Simba, bali kupata punguzo kubwa au kuingia
bure kwenye matukio yanayoandaliwa na Simba na kwenye maduka (yanayouza bidhaa
za Simba) pia yatatoa punguzo kwa watoto wenye kadi hizo,” amesema.
Kajuna amesema upatikanaji wa kadi hizo ni
moja ya majukumu ya kampuni yao waliyoingia na klabu ya Simba kuhakikisha
wanabuni mbinu zitakazoisaidia klabu hiyo kupata mapato.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANACHAMA SIMBA AKIFIWA KULIPWA 250,000/”
Post a Comment