Friday, July 3, 2015

BUNGE LAAHIRISHWA TENA.




SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha bunge baada ya kutokea mzozo kwa wabunge wa upinzani kusimama na kuomba mwongozo wakati Waziri wa Nishati na madini, George Simbachawene alipoanza kusoma kwa mara ya pili Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015).

Baadhi ya wabunge wa upinzani walisimama kuomba mwongozo akiwemo, Tundu Lissu lakini hawakupewa nafasi ndipo wenzao nao waliposimama na kuanza kupaza asauti wakiomba mwongozo.

Spika aliahirisha bunge hilo huku akiwataja kwa majina baadhi ya wabunge wanaodaiwa kuanzisha fujo bungeni.

0 Responses to “ BUNGE LAAHIRISHWA TENA.”

Post a Comment

More to Read