Wednesday, September 30, 2015
MBEYA,TUME YA UCHAGUZI YATOA KAULI YA MATUMAINI.
Do you like this story?
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewahakikishia wananchi na
vyama vya siasa kuwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika ngazi zote za
Udiwani, Ubunge na Urais yatatolewa kwa wakati bila ya mizengwe yoyote.
NEC imesema imejipanga kuhakikisha kuwa hakuna ucheleweshaji
wa matokeo yoyote ya uchaguzi huo kwa kisingizio cha changamoto za mfumo wa
uingizaji matokeo kutoka vituoni.
Uthibitisho huo umetolewa jijini Mbeya na Afisa wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, anayeshughulikia masuala ya uchaguzi, Jane Tungu, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kando ya mafunzo ya siku mbili ya uendeshaji
wa uchaguzi huo kwa Waratibu wa Uchaguzi wa mikoa ya Mbeya na Iringa,
Wasimamizi Wasaidizi na Maafisa wa Uchaguzi wa halmashauri zote za mikoa
hiyo.
Waratibu wa Uchaguzi huo kwa mikoa ya Mbeya na Iringa,
wamewaondoa hofu wananchi kuwa kamwe hawatafanya upendeleo kwa chama chochote
cha siasa kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa bali watazingatia kanuni,
sheria na maadili ya uchaguzi yaliyowekwa na tume.
Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro, amewataka Mawakala wa vyama vya siasa kutambua kuwa jukumu lao ni
kuangalia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
kama zinatekelezwa ipasavyo, lakini hawapaswi kuingilia utendaji wa Maafisa wa
tume na Wasimamizi wa uchaguzi huo.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote
nchini kwa ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA,TUME YA UCHAGUZI YATOA KAULI YA MATUMAINI.”
Post a Comment