Wednesday, September 30, 2015

MPENZI WA MWIGIZAJI JIM CARREY AJIUA BAADA YA 'KUTEMWA'


Cathriona White  akiwa na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwigizaji maarufu wa filamu za Hollywood, Jim Carrey.

White (wa pili kushoto) wakati wa sherehe ya ndoa ya dada yake, Lisa (katikati), mama yao mzazi Brigid (kushoto) na kaka yao, James (kulia).

Nyumba ulimokutwa mwili wa marehemu Cathriona White


Los Angels, Marekani
CATHRIONA WHITE (28) mkazi wa visiwa vya Ireland, Uingereza,  anasadikiwa kujiua baada 'kutemwa' na mpenzi wake ambaye ni mwigizaji maarufu wa filamu za Hollywood, Jim Carrey.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi mjini Los Angeles inasema kuwa usiku wa Jumatatu, marafiki wa Cathriona White walikuta mwili huo kwenye nyumba moja wakati wakimtafuta.

Cathriona anasadikiwa kufa baada ya kunywa madawa kupita kiasi, polisi wa hao wameripoti na kuongeza kwamba pembezoni mwa mwili wa Cathriona  palikutwa masalia ya vidonge vingi hivyo kuwafanya waamini kuwa pengine dawa hizo ndizo zilimtoa uhai.

Siku moja kabla ya kifo chake, Cathriona aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa, “Ninajiondoa kwenye mtandao wa Twitter, nimekuwa mwema kwa marafiki zangu na mpenzi wangu.”

Kwa upande wake,  mwigizaji Jim Carrey (53) alishtushwa na kuumizwa na taarifa za kifo cha aliyekuwa mpenzi wake huyo.  Aliandika ujumbe na kuwatumia ndugu zake kwenye baruapepe akisema, “Nimempoteza Cathriona, siwezi kuamini kilichotokea, nitafanya nini mimi?”
Wapenzi hao waliachana Alhamisi ya wiki jana wakati Cathriona alifariki juzi Jumatatu.

Cathriona na Carrey walianza uhusiano mwaka 2012, lakini baadaye walifarakana na kuachana baada ya miezi michache. Mwaka 2014 walirudiana wakaendelea na mahusiano kwa muda wa wiki mbili tu kabla ya kuachana tena. Mei mwaka huu marafiki hao walirudiana tena kwa mara nyingine ndipo walipokuja kuachana tena wiki jana Alhamisi.

0 Responses to “MPENZI WA MWIGIZAJI JIM CARREY AJIUA BAADA YA 'KUTEMWA'”

Post a Comment

More to Read