Thursday, October 1, 2015
MAN UNITED, CITY ZANG"AA ULAYA.
Do you like this story?
Timu za Jiji la
Manchester, Man United na Man City zimefanyikiwa kupata ushindi wake wa kwanza
katika michuano ya klabu bingwa ulaya msimu huu.
Man United wakiwa katika dimba lao la Old
Trafford walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vfl Wolfsburg, Daniel Caligiuri
alianza kuwaandikia Wolfsburg bao la mapema kabla ya Juan Mata kusawazisha bao
hilo kwa mkwaju wa penati na baadae Chriss Smalling kufunga bao la ushindi.
Man City wakicheza ugenini walipata ushindi
kwa kuichabanga timu ya Borrusia Monchenglabach kwa mabao 2-1 mabao ya City
yakifungwa na Nicolas Otamend na Sergio Aguero huku lile la Borrusia
Monchenglabach likifungwa na Lars Stindl.
Katika mchezo mwingine Real Madrid waliibuka
na ushindi dhidi ya Malmo kwa mabao 2-0 mabao yote yakiwekwa kimiani na
Cristiano Ronaldo na kufanikiwa kufikisha mabao 500 akiwa mchezaji wa soka la
kulipwa.
Matokeo mengine ya klabu bingwa barani ulaya
Shakhtar Donetsk 0 -3vParis St Germaine
CSKA 3-2 PSV
FC Astana 2 -2 Galatasaray
Atletico Madrid 1 -2 Benfica 2
Juventus 2-0 Sevilla
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAN UNITED, CITY ZANG"AA ULAYA.”
Post a Comment