Wednesday, October 7, 2015
LIVERPOOL KUPATA KOCHA MPYA
Do you like this story?
Klabu ya Liverpool
inakaribia kumteua meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Jurgen Klopp.
Majogoo hao wa jiji la Liverpool wanatarajiwa
kukamilisha makubaliano yao siku ya Alhamisi na Klopp raia wa Ujerumani
kuchukua rasmi mikoba ya Brendan Rodgers mwishoni mwa juma hili, kwa mkataba wa
miaka mitatu.
Rodgers alitimuliwa siku ya Jumapili kufuatia
suluhu ya 1-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.
Klopp ameomba kuambatana na wasaidizi wake
wawili wa zamani katika benchi la ufundi ambao ni Zeljko Buvac na Peter
Krawietz.
Buvac raia wa Bosnia mwenye miaka 54 na
mjerumani Krawietz mwenye miaka 43, walitoa ushirikiano mzuri na kupata
mafanikio makubwa wakifanya kazi pamoja klabuni Borussia Dortmund.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LIVERPOOL KUPATA KOCHA MPYA”
Post a Comment