Thursday, October 15, 2015
MWENYEKITI WA NLD, EMMANUEL MAKAIDI AFARIKI DUNIA
Do you like this story?
![]() |
| Dk. Emmanuel Makaidi enzi za uhai wake. |
MWENYEKITI Mwenza wa Ukawa na Mwenyekiti wa
chama cha NLD, Emmanuel Makaidi amefariki dunia leo mchana kwa shinikizo la
damu akiwa Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.
Wasifu wake
Alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani
Masasi mkoani Mtwara. Alianza elimu katika Shule ya Msingi Namalenga wilayani
Masasi kati ya mwaka 1948 – 1952, mwaka 1953 – 1954 alisoma katika Shule ya
Kati (Middle school) iitwayo Luatala hukohuko Masasi.
Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari ya
Chuo cha Mtakatifu Joseph na kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya
mwaka 1953 hadi 1956.
Makaidi alisoma darasa la 13 na 14 (kidato
cha tano na sita) katika Shule ya Sekondari Luhule, Uganda kati ya mwaka 1957 –
1958. Baada ya hapo alielekea Afrika Kusini na kujiunga na Chuo Kikuu cha
Witwatersrand na kuhitimu Shahada ya Uendeshaji na Usimamizi kati ya mwaka 1958
– 1960.
Baada ya kuhitimu vizuri pale Witts,
aliendelea kupata ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili, mara hii alielekea
Marekani na kusoma masuala ya Menejimenti na Utawala kwa ngazi ya uzamili kati
ya mwaka 1960 – 1962.
Alisoma pia katika Chuo Kikuu cha Howard
kilichoko jijini Washington, Marekani. Baada ya kurejea nchini akiwa mhitimu wa
M.A, Makaidi alianza kazi serikalini mwaka 1966 hadi mwaka 1973 akiwa mchambuzi
kazi mkuu, katika kitengo cha Utumishi. Kati ya mwaka 1974 na 1975 (miaka
miwili).
Alirudi tena Marekani na kusoma Shahada ya
Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Howard. Aliporejea
nchini kwa mara ya pili mwaka 1976 aliendelea na kazi yake pale Utumishi hadi
mwaka 1985 alipopewa kazi nyingine kubwa zaidi, akawa Mkurugenzi wa Miundo na
Mishahara kwenye kamati iliyokuwa inashughulikia mashirika ya umma nchini.
Baada ya hapo aliendelea na kazi serikalini
ila kuanzia mwaka 1992 hadi mauti yanamfika, Dk Makaidi hajajishughulisha tena
na kazi za serikalini wala mashirika binafsi.
Alikuwa amejiajiri akiwa na kampuni kadhaa
zilizoajiri Watanzania wa vipato vya kawaida, lakini pia alikuwa akitoa kutoa
ushauri wa kitaalamu kwa kampuni za ndani na nje ya nchi huku akiongoza chama
cha NLD akiwa Mwenyekiti.
Dk Makaidi ni mwandishi mzuri wa vitabu,
ameshaandika zaidi ya vitabu 10. Marehemu ameacha mke aitwaye Modesta Ponela na
walibahatika kupata watoto wanane.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali
pema peponi . AMEN!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “MWENYEKITI WA NLD, EMMANUEL MAKAIDI AFARIKI DUNIA”
Post a Comment