Thursday, October 8, 2015
WATU SABA WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUFELI BREKI JIJINI MBEYA.
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Acp Ahmed Msangi akitoa Taarifa. |
Vibanda vya wafanyabiashara maeneo ya Simike Stand vilivyo pitiwa na Lori hilo mara baada ya kufeli Bleki |
Wananchi wakiwa katika eneo la tukio eneo la Simike Jijini Mbeya. |
TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.10.2015.
WATU
SABA WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUFELI BREKI JIJINI
MBEYA.
WATU SABA WAFARIKI DUNIA BAADA YA LORI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.617 AJP LENYE TELA T.656 BZQ AINA YA SCANIA LILILOKUWA
LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA NCHINI KONGO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE RAMADHAN HASSAN (31) MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM KUACHA NJIA
NA KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU.
WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO WAMETAMBULIKA KWA MAJINA
YA 1. RASHID MWAKIPOLOLO MIAKA KATI YA 17 – 22 2. MTOTO ROSE OSWARD
(07) MKAZI WA SIMIKE 3. MARIAM MWAMEZE MIAKA KATI YA 23 – 25 4.
GRACE MSIMBA (36) MKAZI WA ILEMI 5. FREDRICK MANYILA (17) MKAZI WA
MBOZI NA WATOTO WAWILI, JINSI YA KIUME WENYE UMRI KATI YA MIAKA MITATU HADI
MITANO.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 07.10.2015 MAJIRA YA
SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA SIMIKE, KATA YA MABATINI, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI
WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. HAPPY WENER (31) MKAZI WA SIMIKE NA MTOTO
SHADRACK JOSEPH (04) MKAZI WA SIMIKE AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA AJALI NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI ZA GARI
NA KUPELEKEA DEREVA KUSHINDWA KULIMUDU KUTOKANA NA ENEO HILO KUWA NA MTEREMKO
MKALI. DEREVA AMEKAMATWA, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA MADEREVA/WAMILIKI WA VYOMBO VYA
USAFIRI KUVIFANYIA SERVICE VYOMBO VYAO MARA KWA MARA ILI KUWEZA KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU NA WATUMIAJI
WENGINE WA BARABARA KUEPUKA KUKAA PEMBEZONI MWA BARABARA KWANI NI HATARI KWA
USALAMA WA MAISHA YAO.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU SABA WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUFELI BREKI JIJINI MBEYA.”
Post a Comment