Friday, October 9, 2015
KOCHA MPYA WA LIVERPOOL JURGEN KLOOP ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU
Do you like this story?
Jurgen Klopp amesaini kandarasi ya miaka mitatu
usiku wa jana kuwa kocha mkuu wa klabu ya Liverpool na amepewa jukumu la
kurejesha makali ya majogoo wa jiji katika michuano mikubwa ya Ulaya.
Klopp anatambuliswa asubuhi hii mbele ya waandishi
wa habari na ataongea kwa mara ya kwanza na LIVERPOOL FC TV.
Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 48 anachukua
mikoba yaBrendan Rodgers ambaye alifutwa kazi siku ya Jumapili baada ya
kuiongoza timu hiyo ambayo iko nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza
kwa miaka mitatu na nusu.
Klopp hajakuwa akikufunzi timu yoyote tangu mwezi Mei,wakati
alipomaliza ukufunzi wake wa miaka saba katika klabu ya Borussia Dortmund ya
Ujeruamani ili kuchukua likizo.
Anatarajiwa kumleta Zeljko Buvac na Peter Krawietz,manaibu
wake wa zamani katika klabu hiyo ya Bundesliga ili kujaza safu yake ya
ukufunzi.
MECHI SITA ZA KWANZA ZA KLOPP
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KOCHA MPYA WA LIVERPOOL JURGEN KLOOP ASAINI MKATABA WA MIAKA MITATU”
Post a Comment