Tuesday, November 17, 2015
MAGULI AFURAHIA KUCHEZA NA SAMATTA
Do you like this story?
Kinara wa upachikaji mabao wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara Elius Maguli ambaye amerejea kwa mara ya kwanza kwenye
kikosi cha Stars tangu alipoachwa kwa mara ya mwisho mwaka 2013. Maguli alianza
kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Algeria uliochezwa jijini Dar
es Salaam na kufanikiwa kufunga goli la kwanza kwenye sare ya kufungana magoli
2-2.
Mtandao huu umetaka kujua Maguli alijisikiaje
kurejea tena kwenye kikosi cha Stars na kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi
cha kwanza.
“Kwangu mimi ni furaha kwanza ukizingatia
mwalimu aliniamini na kunipa nafasi, ikabidi na mimi nijiamini ili niweze
kufanya vizuri kama ilivyoweza kutokea”, alisema Maguli wakati akizungumza na
Yahaya Mohamed kabla ya mazoezi ya jana usiku kwa ajili ya kujiandaa na mchezo
wa marudiano dhidi ya Algeria utakaochezwa leo saa tatu usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.
Maguli alipoulizwa anajisikiaje kusimama
mbele kwenye nafasi ya ushambuliaji pamoja na Mbwana Samatta kwenye kikosi cha
Stars alisema kwamba, anafurahi kucheza na Samatta na ushirikiano ndiyo ulizaa
mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Algeria.
“Ushirikiano ni mzuri, kabla ya mchezo
tuliocheza nyumbani kuanza, tulikaa na kuzungumza ni kitu gani tufanye ili
tuweze kupata magoli na kilichotokea ni kile ambacho kila mtu aliona”.
Maguli alionesha kiwango kizuri kwenye mchezo
wa awali uliochezwa jijini Dar es Salaam na huenda leo akawa miongoni mwa
wachezaji ambao wataanza kwenye kikosi cha kwanza wakati Stars itakapokuwa
ikikabiliana na Algeria kwenye mchezo wa marudiano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAGULI AFURAHIA KUCHEZA NA SAMATTA”
Post a Comment