Tuesday, November 17, 2015
MADRID, MSIYEMPENDA KAJA!
Do you like this story?
Zikiwa zimebaki siku nne kuelekea mchezo wa
mahasimu wakubwa wa soka la Hispania, El Classico inayowakutanisha miamba
yasoka Real Madrid na Barcelona, Lionel Messi ameanza mazoezi Jumatatu hii
tayari kwa mechi hiyo.
Habari hizi sio za kufurahisha kwa mashabiki
wa Real Madrid ambao wasingependa kukutana na Barcelona hii yenye Lionel Messi
ndani huku pia Ivan Rakitic naye akitajwa kuwa fit baada ya kupona majeraha
yake.
Mchezaji Lionel Messi ambaye alikaa nje ya
uwanja, tangu alipoumia mwishoni kwa mwezi September Barcelona ikicheza dhidi
ya Las Palma’s anatarajiwa kucheza katika mchezo huo utakao pigwa Santiago
Bernabeu uwanja wa Real Madrid Jumamosi hii.
Barcelona haikuoekana kuyumba sana baada ya
kukosekana kwa nyota huyo, ujio wake ni habari za faraja kwa mashabiki wa Barca
na kocha wao Luiz Enrique ambao sasa watakua wanaombea kuona mchezaji huyo
anarudia kiwango chake pamoja na kuwa alikua nje ya uwanja kwa takribani miezi
miwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MADRID, MSIYEMPENDA KAJA!”
Post a Comment