Wednesday, November 18, 2015
DOYE MOKE : BARTHEZ ALIKUA MZEMBE, STARS INAHITAJI WACHEZAJI WA KIMATAIFA ZAIDI
Do you like this story?
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam
Baada ya kushuhudia timu ya kandanda ya Tanzania ikichapwa kipigo ‘kikubwa zaidi’ tangu ilipojiunga FIFA mwaka 1964, wadau mbalimbali wamejitokeza na kuweka wazi hisia zao. Taifa Stars ilifungwa 7-0 na Algeria usiku wa jana Jumanne ikicheza ugenini na hivyo kuondolewa katika hatua ya pili kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia nchini Urussi.
Baada ya kushuhudia timu ya kandanda ya Tanzania ikichapwa kipigo ‘kikubwa zaidi’ tangu ilipojiunga FIFA mwaka 1964, wadau mbalimbali wamejitokeza na kuweka wazi hisia zao. Taifa Stars ilifungwa 7-0 na Algeria usiku wa jana Jumanne ikicheza ugenini na hivyo kuondolewa katika hatua ya pili kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia nchini Urussi.
Kipigo cha jumla cha mabao 9-2 kimewaacha
‘wazi’ kila mmoja na sasa naamini Tanzania ina safari ndefu kufikia kufuzu kwa
michuano mikubwa. Mara ya mwisho kwa Stars kufuzu kwa fainali kubwa ni mwaka
1980 katika fainali za mataifa ya Afrika nchini Nigeria. Baada ya hapo, kizazi
hadi kizazi hakuna kipya walichoweza kufanya.
Kufuzu kwa CHAN 2009 michuano ya kwanza kwa
Mataifa ya Afrika inayohusisha wachezaji wa ndani ya Afrika pekee ilikuwa ni
kama ‘bahati ya mtende’ lakini ghafla timu haikudumu katika ubora wake na
ikapotelea mbali.
Kizazi hiki cha sasa ambacho kinawajumuhisha
washindi pekee wa klabu bingwa Afrika, Thomas Ulimwengu na mfungaji bora wa
michuano ya klabu Afrika, Mbwana Samatta ndiyo kimejikuta katika historia mbaya
zaidi kimpira.
Hakuna unachoweza kusema sasa, labda ni
kukubali tu udhaifu wa ligi kuu ya Tanzania bara ambayo ‘watawala’ wake Yanga
SC, Azam FC na Simba SC ndiyo wamekuwa wakiunda sehemu kubwa ya timu ya Taifa.
Wakati huu wachezaji wa Kitanzania wakiwa wameanza kutawanyika nje ya mipaka ya
nchi, maofisa wa TFF na wakufuzi wa timu wameshindwa kuhakikisha wanapatikana
wakati Stars inapobaliwa na gemu za kimataifa.
Abdi Kassim, Hamis Mroki, Juma Ndanda Luinzo,
Uhuru Suleiman, Mrisho Ngassa, Ulimwengu na Samatta hawa ni baadhi wachezaji wa
Kitanzania wanaocheza nje ya nchi lakini ni watatu tu wanaojumuhishwa katika
timu. TFF na walimu wanaamini kuwa wachezaji wanaocheza VPL ni wazuri zaidi
lakini mpira wa kimataifa unahitaji pia mbinu mpya kiuchezaji kila wakati hasa
kwa wachezaji.
Kama tunahitaji vijana watu waende kucheza
nje ya nchi basi tuwe tayari pia kuwaita katika timu ya Taifa kwa kuwa ni sifa
pia kwa mchezaji klabuni kwake, inamuongezea uwezo, heshima na msaada wake
uwanjani huwa mkubwa kuliko mchezaji bora wa VPL.
“Mimi binafsi nafahamu kiundani soka la
bongo, katika ufahamu wangu, mchezaji wa kibongo au coach wa kibongo wanatabia
moja. M-bongo akiwa ndani ya Tanzania ni mjanja kwa kila kitu, akitoka nje ya
Tanzania anakua mdogo sana kwa kila kitu.” Anaanza kusema mlinda mlango wa
zamani wa Simba SC na Yanga SC , Doy Moke
“Taifa Stars ilipoteza mchezo kutokana na
kutokujiamini, woga, hasa mimi binafsi lawama zote na mpa Barthez (kipa Ally
Mustapha) kwa kufungwa magoli ya kizembe mno hasa dakika ya kwanza. Kwa uzoefu
wangu timu ilicheza ugenini mwenye jukumu la kuibeba timu ni kipa anapaswa
kucheza zaidi ya asilimia 60 kwa kuibeba timu na kuwapanga mabeki wake”.
“Nakumbuka nilivyokua Yanga mwaka 2001
tulienda Bulawayo kucheza ugenini kabla ya mechi kuanza kila mchezaji wetu
alipanic, Mahadhi akanifata na kuniomba tusifungwe magoli mengi, bora
nijitahidi tufungwe machache, nilivyo mtazama usoni nikaona alikua akitetemeka.
“Nilimwambia hakika hatutafungwa hâta goli 1,
hakuniamini, lakini game ilivyo anza walitushambulia kuanzia dakika ya kwanza
mpaka ya ishirini niliokoa hatari zote kwa ujasiri, timu yote ikajenga imani
kwangu, nakurudi katika game, mwisho tulishinda 2-0 ugenini.” Anasimulia Moke
“Wachezaji wengi wa kibongo huchukulia mpira
kama mwajiriwa wa kampuni fulani, hana mpango wakujiendeleza, bora afanye
mazoezi na aoneshe nidhamu basi. Football ni zaidi ya hiyo. Kuletwa kwa
wachezaji wakigeni kumeifanya Tanzania angalau mpira uanze kuchezwa, lakini kwa
wachezaji wakibongo wanaocheza VPL safari bado ni ndefu mno kwao.
“Niliona hayo ujasiri wa timu ya taïfa ya
Burundi (Jumatatu hii) walicheza mbele ya watu laki moja (100,000) uwanjani wa
Stade de Martyrs, Kinshasa, walicheza vizuri mno nakuunyamazisha umati mkubwa
kwa kupata matokeo ya goli 2-2 ugenini.
“Kwa Tanzania bora wachezaji wa cheze nje ya
Tanzania, na ma-coach hivyo hivyo. Bila hivyo mh!, Yanga kabla hawajaingia
Champions Leagues watafute golikipa jasiri, bila ivyo itakua kazi bure”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DOYE MOKE : BARTHEZ ALIKUA MZEMBE, STARS INAHITAJI WACHEZAJI WA KIMATAIFA ZAIDI”
Post a Comment