Thursday, November 12, 2015

MATOLA: KERR AMENIONDOA SIMBA




Kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola jana usiku aliandika barua kwa ajili ya kuomba kujiuzulu kuifundisha kikosi cha Simba.

Suleiman Matola ambaye amekuwa kocha Msaidizi wa kikosi cha Simba kwa muda mrefu baada ya kuitumikia Simba kama mchezaji na nahodha.

Uamuzi wa Matola kujiuzulu umeridhiwa na kamati tendaji ya Uongozi wa Simba ambayo inaamini kwa dhati umuhimu wa kumpa kocha mkuu uhuru wa maamuzi anayoyaona yanafaa katika kuleta tija kwake na timu.

Kocha Matola amefanya uamuzi huu yeye mwenyewe wa kujitoa kuifundisha timu ambayo pia ilishiriki katika kukuza uwezo wake wa ukocha.

Akizungumza na simbasports.co.tz Rais wa Simba Evans Aveva alisema uongozi mzima wa Simba unasikitishwa na uamuzi wake lakini pia unapenda kumtakia kila la kheri katika ufundishaji wa Soka. SIMBA NGUVU MOJA

0 Responses to “MATOLA: KERR AMENIONDOA SIMBA”

Post a Comment

More to Read