Thursday, November 5, 2015

MEXICO YAHALALISHA BANGI ITUMIKE KWA WATU WANNE TU


Mahakama Kuu nchini Mexico.

Mmea wa zao la bangi.

Mmoja wa wanaharakati na watumiaji wa zao la mmea wa bangi.

Mwanaharakati anayeunga mkono matumizi ya bangi nchini Mexico, Lucha Libre aliyevaa Maski, akishangilia mara baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuruhusu matumizi ya bangi.

Mmoja wa wavuta bangi raia wa Mexico akivuta msokoto wa bangi nje ya jengo la Mahakama Kuu ya nchi hiyo jana.



Mahakama Kuu nchini Mexico imehalalisha zao la bangi litumike kwa kundia la watu wane tu ambao ni wanaharakati nchini humo. Watu hao wane wameruhusiwa kupanda na kusambaza bangi kwa matumizi yao wenyewe.

Hata hivyo sheria hiyo imetoa rukhsa kwa watu hao wane pekee ambao ndiyo walikwenda mahakamani hapo kuomba waruhusiwe kupanda na kutumia bangi.

Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa sheria hiyo huenda ikafungua milango itakayoruhusu na kuhalalishwa matumizi ya bangi kwa jamii yote nchini humo siku zijazo.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kuwa sharia hiyo hiyo inazua mjadala kuhusu njia za kudhibiti matumizi ma usambazaji wa madawa ya kulevya.

Wanaharakati wanasema kuwa kushindwa kwa Mexico kuhalalisha matumizi ya bangi ndiko kulikowawezesha walanguzi wa mihadarati kukolea katika biashara hiyo na kujivunia mabilioni ya fedha.

0 Responses to “MEXICO YAHALALISHA BANGI ITUMIKE KWA WATU WANNE TU”

Post a Comment

More to Read