Thursday, November 5, 2015
DKT MAGUFULI AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Do you like this story?
Hatimaye, Dkt.
John Magufuli ameapishwa rasmi na kuwa Rais wa serikali ya awamu ya Tano ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania akihitimisha rasmi uongozi wa serikali ya awamu
ya nne iliyoongozwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Rais Magufuli
na makamu wake Bi. Samia Suluhu wamekula kiapo leo katika sherehe zilizofanyika
katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mbele ya viongozi wa nchi
mbalimbali pamoja na viongozi wa chama, serikali na viongozi wa dini ambazo
zilinogeshwa zaidi na gwaride la Jeshi la Wananchi.
Dkt. Magufuli ameapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Othman Chande na kupigiwa mizinga 21 ya heshima baada ya kukabidhiwa kijiti cha uongozi na rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Katika Jukwaa la Kiapo, walikuwepo Jaji Mkuu, Othman Chande, Katibu Mkuu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Spika wa Bunge la 10, Bi. Anne Makinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wengine
waliokuwa katika jukwaa la Kiapo ni pamoja na Rais wa serikali ya awamu ya nne,
Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, Dkt. Gharib Ali
Bilal, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Shein.
Rais wa awamu
ya nne, alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalum la jeshi la Wananchi
kama ishara ya kumuaga kwa heshima na kuteremsha bendera yake, kabla
hajakabidhi madaraka kwa rais mpya Dkt. Magufuli.
Pia, viongozi
wa dini za aina Tatu walihusika katika kuunda jopo la kiapo na kutoa sala zao
kuliombea Taifa na Rais Mpya, Dkt. John Magufuli.
Marais wa nchi
mbalimbali waliohudhuria ni pamoja na Paul Kagame (Rwanda), Jacob Zuma (Afrika
Kusini), Robert Mugabe (Zimbabwe), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoel Museven
(Uganda), Rais wa Msumbiji pamoja na mawaziri wa nchi mbalimbali.
Sherehe hizo
zilihudhuriwa na maelfu ya wananchi na kupata baraka ya mvua wakati wote lakini
wananchi hao waliendelea kufuatilia tukio hilo la kihistoria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ DKT MAGUFULI AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA”
Post a Comment