Thursday, December 31, 2015
MKUU WA MKOA WA MBEYA AHIMIZA USHIRIKIANO WA KISEKTA ILI KUKOMESHA KIPINDUPINDU
Do you like this story?
| Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya mlipuko wa Kipindupindu(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
| Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina |
| Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mbeya wakipatiwa semina kutoka wizara ya Afya juu ya kuelimisha wananchi kuhusu mlipuko wa Gonjwa la Kipindupindu(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
| Dr Vincent Asseu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya kutoa Huduma za kinga na afya akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari jijini Mbeya |
| Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mbeya wakipatiwa semina kutoka wizara ya Afya juu ya kuelimisha wananchi kuhusu mlipuko wa Gonjwa la Kipindupindu(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Kwaajili
ya kupambana na tatizo la kipindupindu mkoani Mbeya, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas
Kandoro amezitaka sekta mbalimbali kuungana pamoja na kuchukua hatua stahiki
ili kulimaliza tatizo hili.
Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Mbeya Kandoro amesema kuwa kwa kuwa suala la
kukabiliana na kipindupindu ni mtambuka basi sekta zote ikiwa ni pamoja na
Maji, Elimu, Maendeleo ya jamii, Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi hazina budi
kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu mkoani Mbeya.
Aidha amesema kuwa wizara husika itaendelea
kufanya tathmini ya hatua zinazochukuliwa ili hatua stahili zichukuliwe
kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.
Ni
vema kukukumbusha kuwa tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 193 katika mkoa
wa Mbeya walipata ugonjwa huu kuanzia novemba 27, 2015 ambapo kati ya hao ni
watu 6 waliopoteza maisha kufuatia ugonjwa huo ambayo ni sawa na asilimia 3.1
ya waliougua. Kwa mujibu wa mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya, wilaya iliyopatikana
kuwa na wagonjwa wengi tangu mlipuko uanze ni Kyela iliyokuwa na jumla ya
wagonjwa 187 sawa na 97% ikifuatiwa na Ileje iliyopatikana kuwa na wagonjwa 6
sawa na 3% ya wagonjwa wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AHIMIZA USHIRIKIANO WA KISEKTA ILI KUKOMESHA KIPINDUPINDU”
Post a Comment