Monday, January 4, 2016
KERR AMTOA ANGBAN KIKOSINI SIMBA
Do you like this story?
Omary Mdose na Said Ally
KOCHA Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema katika harakati zake za kuutetea ubingwa wa Kombe la Mapinduzi hatamtumia kipa wake, Muivory Coast, Vincent Angban.
KOCHA Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema katika harakati zake za kuutetea ubingwa wa Kombe la Mapinduzi hatamtumia kipa wake, Muivory Coast, Vincent Angban.
Angban kwa siku za hivi karibuni ameonekana
kukaa langoni katika kila mchezo wa Simba kwenye Ligi Kuu Bara kitendo ambacho
kimemfanya kocha huyo kumpumzisha na badala yake kuwatumia Peter Manyika na
David Kissu.
Katika michuano hiyo ambayo msimu uliopita Simba
ikiwa chini ya Mserbia, Goran Kopunovic iliutwaa ubingwa huo, msimu huu Kerr
amepanga kuwatumia zaidi wachezaji wasiokuwa na nafasi kikosini hapo akiwemo
Novatus Lufunga, Mohammed Fakhi, Issa Said na wengine.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kerr amesema
Manyika amekuwa akionyesha kiwango cha hatari mazoezini hali inayomfanya
kumkabidhi mikoba yote ya Kombe la Mapinduzi akisaidiana na chipukizi, Kissu.
“Kiukweli Manyika amekuwa akijitahidi sana
mazoezini, siku hadi siku naona kiwango chake kinakua, hivyo nimepanga kumtumia
kwa muda wote kwenye michuano ya Mapinduzi akisaidiana na Kissu, kwa upande wa
Angban yeye nitampumzisha.
“Michuano hii sijaitilia maanani sana kama
ilivyo ligi kuu, lakini si kwamba naidharau, bali nitapambana kuhakikisha
ubingwa wetu tunautetea, nawaamini vijana wangu, hawataniangusha,” alisema
Kerr.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ KERR AMTOA ANGBAN KIKOSINI SIMBA”
Post a Comment