Monday, January 4, 2016
TWITE APEWA CHEO KIPYA YANGA
Do you like this story?
Hans Mloli,Dar es Salaam
UONGOZI wa benchi la ufundi la Yanga umempa cheo cha unahodha, kiungo wa timu hiyo Mbuyu Twite baada ya Haruna Niyonzima kutemwa klabuni hapo.
UONGOZI wa benchi la ufundi la Yanga umempa cheo cha unahodha, kiungo wa timu hiyo Mbuyu Twite baada ya Haruna Niyonzima kutemwa klabuni hapo.
Awali kabla ya Niyonzima ambaye pia ni
nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda kupewa wadhifa huo cheo hicho kilikuwa
mikononi mwa Twite, hivyo hii ni mara ya pili kwa kiraka huyo kuchukua nafasi
hiyo.
Twite anatazamiwa kutumia nafasi hiyo
kuiongoza Yanga kwenye michezo yote ya Kombe la Mapinduzi na ile ya awali baada
ya kurejea kwa Ligi Kuu Bara kutokana na nahodha mkuu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
kuwa majeruhi.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, ameliambia
Championi Jumatatu kuwa, cheo hicho kipo kwa Twite kwa muda tu kwa kuwa bado
benchi la ufundi chini ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm, halijachagua nahodha
msaidizi mpaka sasa.
“Twite kwa sasa ndiye anaongoza timu kama
nahodha msaidizi baada ya Niyonzima kutemwa, ila atafanya hivyo kwa muda maana
bado hajateuliwa nahodha mpya msaidizi atakayesaidiana na Cannavaro,” alisema
Saleh.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ TWITE APEWA CHEO KIPYA YANGA”
Post a Comment