Monday, January 4, 2016
HALL HANA MPANGO NA MAPINDUZI CUP ZAIDI YA KUTALII TU ZENJ
Do you like this story?
![]() |
| Stewart Hall (kulia) kocha mkuu wa timu ya Azam FC |
Kweli ukisema cha nini wenzio wanasema
watakipata lini, hivi ndivyo unaweza kuichukulia kauli iliyotolewa na kocha
mkuu wa Azam FC Stewart John Hall juu ya michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea
visiwani Zanzibar.
Raia huyo wa England amesema michuano ya
Mapinduzi kwake si lolote si chochote ndiyo maana amewapumzisha wachezaji wake
wengi wa kikosi ambacho kimezoeleka kuanza na kuwapa nafasi wachezaji ambao
wamekuwa hawana nafasi kubwa kwenye timu hiyo.
Hall amesema kombe la Mapinduzi kwake sio
kitu wala halipo kwenye mipango yake badala yake akasema mataji yanayomuumiza
kichwa ni ligi ya Vodacom Tanzania bara, kombe la FA (Azam Sports Federationa
Cup) pamoja na kombe la shirikisho barani Afrika.
“Tumejiandaa kwa ajili ya Vodacom Premier
League, Azam Sports Federation Cup (FA) pamoja na Confederation Cup lakini siyo
Mapinduzi na hiyo imepelekea kubadili wacheaji 10 na kama kuna wa kulaumiwa
basi ni mimi lakini siyo wachezaji”, amesema Hall ambaye anaonekana hana mpango
kabisa na michuano ya Mapinduzi.
“Michael Balou amekwenda kwao kwenye msiba,
Agrey Morris, Kapombe na Erasto Nyoni wao ni majeruhi, Farid Mussa anaenda
Ulaya na nikaamua kumpumzisha Wawa kwasababu anatumika sana karibu kwenye kila
mechi”.
Mchezo wa Azam FC vs Mtibwa Sugar, Hall
aliwaanzisha kwenye benchi Ivo Mapunda, Jean Mugiraneza, Kipre Tchethe, John
Bocco, Frank Domayo ambao wengi wao mara nyingi wamezoeleka kuonekana kwenye
kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “HALL HANA MPANGO NA MAPINDUZI CUP ZAIDI YA KUTALII TU ZENJ”
Post a Comment