Monday, January 4, 2016
DIAMOND ATAJWA TENA TUZO 3
Do you like this story?
MWAKA ameufungua vizuri staa wa muziki
wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya kutajwa kuwania tuzo tatu za
Trends Loaded Music, Too Exclusive pamoja na Hipipo Music.
Katika Tuzo za Hipipo Music ambazo
hutolewa nchini Uganda na Nigeria, Diamond amefanikiwa kuingia katika
vipengele vitatu ambavyo ni East African Super Hit, East african Best
Video pamoja na Best African Artist of the Year.
Kwa upande wa Tuzo za Xclusive Music, Diamond ameingia katika kipengele kimoja cha Best African Artist of the Year.
Katika Tuzo za Trends Loaded Music, Diamond napo ameingia katika kipengele kimoja cha African Artist of the Year.
Tuzo hizo zote zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ DIAMOND ATAJWA TENA TUZO 3”
Post a Comment