Monday, January 4, 2016
TFF KATIKA TUHUMA NYINGINE NZITO, ACHANA NA ILE YA KUKWEPA KODI
Do you like this story?
Kweli soka la bongo ni kizungumkuti, waamuzi
wanaochezesha liki kuu ya Voidacom Tanzania bara wamefichua ‘jipu’ jingine
ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) safari hii siyo lile la
kudaiwa kodi na TRA bali jipu hili ni la kudaiwa posho na baadahi ya waamuzi wa
VPL.
Waamuzi waliochezesha mchezo kati ya Coastal
Union dhidi ya Stand United uliochezwa December 26, 2015 hawajapewa posho zao
hadi sasa huku waamuzi hao wakitakiwa kujigharamia usafiri, chakula pamoja na
malazi.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface
Wambura kupitia gazeti moja la michezo alikanusha taarifa za bodi yake kudaiwa
na waamuzi hao, akisema hakuna mwamuzi anayeidai bodi yake.
Mmoja wa waamuzi ambaye ni miongoni mwa
waliochezesha mechi ya Coastal Union vs Stand United amezungumza na mtandao huu
kwa sharti la kutoandikwa jina lake amemesema bado hawajalipwa pesa za mchezo
huo uliochezwa tarehe 26. 12. 2015.
“Nimesoma gazeti la Champion, Wambura anasema
hakuna referee anayedai lakini mpaka leo sisi hatujalipwa tumechezesha mchezo
kati ya Coastal Union na Stand United tarehe 26. 12. 2015”, alisema mwamuzi
huyo ambaye alitoa tahadhari ya kutoandikwa jina lake.
Kwa mwenendeno huu, je TFF inaweza kupambana
na suala waamuzi kupokea rushwa na upangaji matokeo?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “TFF KATIKA TUHUMA NYINGINE NZITO, ACHANA NA ILE YA KUKWEPA KODI”
Post a Comment