Thursday, December 24, 2015
.SERIKALI YAITANGAZA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI KUWA SIKU RASMI YA USAFI NCHINI
Do you like this story?
| Mbeya |
Serikali
imeitangaza rasmi siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya
usafi na kwamba hatua za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa kwa watendaji
wowote watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.
Agizo hilo
limetolewa jijini Dar es Salaam na naibu waziri wa ofisi ya makamo wa rais,
muungano na mazingira Bw Luoga Mpina ambapo amesema agizo hilo linaanza mara
moja huku akisisitiza kuwa lengo kubwa ni kupambana na magonjwa yanaweza
kusababishwa na uchafu.
Kuhusu athari
za mabadiliko ya tabia nchi waziri Mpina amesema Tanzania hupoteza zaidi ya heka
laki nne za misitu kila mwaka huku joto la dunia likiongeza kwa nyuzi joto
0.85, ambapo pia kina cha bahari kikiongeka hadi kufikia 19 cm, pia akatumia
fursa hiyo kutoa agizo kwa halimashauri zote nchini.
Kwa mujibu wa
taarifa za wizara hiyo ya makamo wa rais muungano na mazingira, Tanzania
inazaidi ya hekta milioni 48.1 za misitu ambayo hutumika kumeza hewa ya kabon
tirion 9.03 ambapo juhudi za upandaji miti zikitajwa kusaidia kuondoa athari za
mabadiliko ya tabia nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “.SERIKALI YAITANGAZA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI KUWA SIKU RASMI YA USAFI NCHINI”
Post a Comment