Friday, December 25, 2015
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATANGAZO YANAYOHUSU TIBA ASILI
Do you like this story?
![]() |
| Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akiwa na Naibu Waziri Wa Afya Hamis Kigwangala. |
Taarifa kutoka
Wizara ya Afya kuanzia tarehe 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote
yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii.
Wale wote wenye
vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba
Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
Utoaji wa elimu
ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala
kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo
utaratibu mwingine utakapotangazwa.
Watoa huduma za
tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza
nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia jana Desemba 2015.
Baadhi ya
nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za
kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na
tiba mbadala
Baraza la Tiba
Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia jana
24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zinazohusu usajili wa watoa huduma,
usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za
tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili
wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.
Taarifa hii
imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John,
Kaimu Katibu Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “ SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATANGAZO YANAYOHUSU TIBA ASILI”
Post a Comment