Friday, December 25, 2015
WATOTO 23 WAZALIWA KWENYE SIKUKUU YA CHRISMASI MBEYA
Do you like this story?
|
Mwanaidi Alphani mkazi wa
Ilomba akiwa amemshika mtoto wake wa kiume kwa furaha(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
|
| Mwenekano wa lango kuu la kuingilia Hospitali ya Wazazi Meta(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
|
NA
SAMWEL NDONI, MBEYA
JUMLA
ya watoto 23, wamezaliwa usiku wa kuamkia
mkesha wa krisimasi katika hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya kitengo cha huduma ya wazazi na
mtoto Meta.
Muuguzi
wa zamu wa hospitali hiyo Fatuma Mkinga alisema kuwa kati ya watoto hao wakiume
ni 13 na wa kike ni 10 na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
Mkinga
amesema kuwa kati yao watoto 12, walizaliwa kwa njia ya kawaida na 11,
walizaliwa kwa njia ya upasuaji na wazazi wao wamelazwa katika hospitali hiyo
wakiwa chini ya uangalizi.
“Tangu
usiku wa kuamkia leo (jana), mpaka muda huu jumla ya watoto 23, wamezaliwa kati
yao wakiume ni 13 na wakike ni 10 wote hali zao ni nzuri, pia wapo waliozaliwa
kwa njia ya oporesheni” alisema.
Baadhi
ya wanawake waliojifungua hospitalini hapo wamesema kuwa wanajisikia vizuri
kujifungua siku aliyozaliwa yesu huku wakielezea kuridhishwa na huduma
waliyopatiwa na madaktari pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo.
“Najisikia
vizuri kujifungua mtoto wangu wa kwanza wa kiume siku ya leo (jana),
nimejifungua salama kwa njia ya kawaida namshukuru Mungu kwa hilo” alisema
Mwanaidi Alphani mkazi wa Ilomba jijini hapa.
Naye
Tumpe Nyalile, mkazi wa Nzovwe aliyejifungua kwa njia ya oparesheni amesema
kuwa anaridhishwa na huduma aliyoipata
kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo kuanzia hatua ya mwanzo.
“Najisikia
vizuri kujifungua siku ya leo, nawashukuru madaktari na manesi kwa huduma nzuri
waliyonipatia, nimejifungua mtoto wa kike nitampatia jina la mariamu,jina la
mama yake yesu ambaye naye tunaamini alijifungua siku kama ya leo”amesema
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “WATOTO 23 WAZALIWA KWENYE SIKUKUU YA CHRISMASI MBEYA”
Post a Comment