Tuesday, March 15, 2016
TAARIFA MPYA NA MUHIMU KWAKO KUTOKA IKULU.
Do you like this story?
Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi,
2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli
awapunguzia ulinzi marais wastaafu".
Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza
kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na
imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio
za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu
wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-15 Machi, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TAARIFA MPYA NA MUHIMU KWAKO KUTOKA IKULU.”
Post a Comment