Saturday, April 2, 2016
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AAHIDI NEEMA KWA WAENDESHA BODABODA
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria
maarufu kama Bodaboda mkoani Dar na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha
kupitia biashara hiyo.
Pamoja na mambo
mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya
shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia
wazimiliki wao.
Katika hatua
nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri utakaowawezesha
bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.
Mwakilishi wa
Bodaboda, Daud Laurian alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni zuio la
kuingia mjini (CBD) la Machi 3,2014.
“Tumekutana
na changamoto nyingi, kwa mfano kutozwa faini kuanzia Sh50,000 hadi zaidi ya
400,000, kukamatwa kinyama na kufukuzwa na magari,” alisema.
Ahadi ya
Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John
Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
Juzi, Meya mpya
wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha
Bodaboda wanaweza kuingia mjini kwa utaratibu maalum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AAHIDI NEEMA KWA WAENDESHA BODABODA ”
Post a Comment