Saturday, April 2, 2016
Polisi Jijini Mwanza Waamuru Kaburi la Marehemu Lifukuliwe ....Ni Baada ya Uongozi wa Hospitali Kukosea na Kukabidhi Maiti ya Mtu Mwingine
Do you like this story?
Polisi mkoani
Mwanza, ndugu, jamaa na marafiki, juzi, walilazimika kufukua kaburi na kutoa
mwili wa Gelinde Masumbuko baada ya kuzikwa na ndugu wa marehemu Said Mussa na
kukaa kaburini kwa siku mbili.
Hatua hiyo
ilifikiwa baada ya wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya
Mkoa wa Mwanza wa Sekou-Toure, kuukabidhi mwili wa Masumbuko kwa ndugu wa
Mussa.
Baada ya
kukabidhiwa mwili huo, ndugu wa Mussa waliendelea na taratibu na kuuzika katika
makaburi ya Nyashana wilayani Ilemela, kabla ya ndugu wa Masumbuko kubaini kuwa
mwili wa ndugu yao uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
hauonekani.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema walilazimika kuingilia kati suala
hilo baada ya ndugu wa Masumbuko kuripoti tukio la mwili wa ndugu yao kupotea
katika mazingira ya kutatanisha.
“Baada
ya uchunguzi kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali tulibaini yalifanyaka
makosa kwa mwili huo kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu Mussa ambao tayari
walishauzika,” alisema.
Uchunguzi huo
ulibaini mwili wa Mussa ulikuwa bado umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi
maiti cha hospitali hiyo.
“Ilibidi
taratibu za kisheria zichukuliwe na mwili wa marehemu Masumbuko kufukuliwa na kukabidhiwa
kwa ndugu zake, huku ndugu wa Mussa nao wakichukua mwili wa ndugu yao kwa
mazishi mapya,” alisema Kamugisha.
Mkanganyiko huo
ulitokea baada ya ndugu wa Masumbuko kutoka Sengerema kufuata mwili katika
hospitali hiyo na kuukosa, hali iliyowalazimu kufuatilia ili kujua alikozikwa
na taratibu za kuufukua zifuatwe.
Ndugu wa
Masumbuko, Finias Elias, alisema walitarajiwa kumzika jana nyumbani kwao
wilayani Sengerema.
Ndugu wa
marehemu Mussa, Said Mussa alisema waliotumwa kuuchukua mwili wa marehemu
walishindwa kumtambua kutokana na kuvimba uso.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Polisi Jijini Mwanza Waamuru Kaburi la Marehemu Lifukuliwe ....Ni Baada ya Uongozi wa Hospitali Kukosea na Kukabidhi Maiti ya Mtu Mwingine ”
Post a Comment