Monday, May 16, 2016
POLISI WATOA TAARIFA KUHUSU BOMU LILILOONEKANA OLD TRAFFOD
Do you like this story?
Ligi Kuu ya Uingereza
(EPL) ilikuwa imalizike Jumapili kwa michezo 10 kupigwa lakini katika mchezo wa
Manchester United na Bournemouth uliokuwa ukitaraji kupigwa Old Trafford
ulihairishwa kutokana na sababu za kiusalama.
Sababu ya kuhairishwa
ni kuonekana kwa kitu ambacho kilidhaniwa kuwa ni bomu la mlipuko hivyo mchezo
ukahairishwa ili kuzuia madhara ambayo yangeweza kujitokeza iwapo bomu hilo
lingelipuka hivyo mchezo ukasimamishwa na mashabiki kutolewa uwanjani kwa
usalama ili kuhakikisha hakuna madhara ambayo yatajitokeza.
Baada ya kufanyika
uchunguzi kumeonekana kuwa halikuwa bomu kama ilivyodhaniwa hapo awali.
Kilichokutwa ni kifaa
ambacho kinatumika kufanya mazoezi ili kuonyesha kama wanyama wanaotumika
katika usalama wanauwezo wa kutambua kitu kilichokuwa ni mlipuko au sio
mlipuko.
Inasemekana kuwa
kifaa hicho kiliachwa na moja ya kampuni ambayo ilikuwwa ikifanya mazoezi
karibu na eneo hilo hivyo wakati wakiondoka wakasahau kuchukua kifaa hicho
ambacho baada ya watu wa usalama kukipata walikiharibu kwa tahadhari kama
linaweza kutokea jambo lolote ambalo sio la kiusalama.
Aidha baada ya
taarifa hiyo, tayari kumetolewa taarifa kuwa mchezo wa Manchester United na
Bournemouth utachezwa siku ya Jumanne saa 4 usiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ POLISI WATOA TAARIFA KUHUSU BOMU LILILOONEKANA OLD TRAFFOD”
Post a Comment