Sunday, May 15, 2016
UINGEREZA KUSAIDIA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI.
Do you like this story?
Miezi
michache baada ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) kujitoa
kusaidia Tanzania katika usambazaji wa umeme vijijini, Serikali ya Uingereza
kupitia taasisi yake ya Energy Africa Initiative, imetangaza utayari wa kutoa
msaada huo.
Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ameeleza utayari huo mwishoni mwa wiki, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliye nchini humo kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani. Katika mazungumzo hayo, Greening alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake wa kupeleka umeme vijijini.
“Tuko
tayari kuwasaidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa
Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Uingereza (DFID),” alisema.
Pia Waziri
huyo wa Uingereza, alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya
Tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko
maalumu wa kushiriki mkutano huo, kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi
zinazofanywa na Serikali ya Rais Magufuli.
Aidha,
alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya Awamu ya
Tano imeionesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda.
Nguvu
mpya Rea
Hatua hiyo ya Uingereza, imekuja wiki moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Alhamisi wiki ijayo, ambayo mjadala wake utafanyika kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa, unatarajiwa kuibua hoja ya kufutwa kwa msaada huo wa MCC wa Dola za Marekani milioni 472, uliokuwa utumike kusambaza umeme vijijini.
Hatua hiyo ya Uingereza, imekuja wiki moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Alhamisi wiki ijayo, ambayo mjadala wake utafanyika kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa, unatarajiwa kuibua hoja ya kufutwa kwa msaada huo wa MCC wa Dola za Marekani milioni 472, uliokuwa utumike kusambaza umeme vijijini.
Mbali na
mjadala huo ambao unatarajiwa kung’ang’aniwa na Kambi ya Upinzani Bungeni,
hatua hiyo ya Uingereza itaongeza nguvu katika jitihada za Serikali
zilizokwishaanza kwa mafanikio za kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika.
Taarifa za
Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) zinaonesha kuwa, pamoja na MCC kujitoa Machi
mwaka huu katika usambazaji umeme, Serikali katika Bajeti ya 2015/ 2016
inayoisha Juni mwaka huu, ilikuwa imeshatenga Sh bilioni 950 kwa ajili ya mradi
wa Rea Awamu ya Pili.
Mradi huo
wenye lengo la kufikisha umeme kwa vijiji 2,500 na kuunganishia nishati hiyo
wateja 250,000 nchi nzima, unatarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu na kupisha
kuanza kwa Rea Awamu ya Tatu, ambayo itaanza Julai mosi na kumalizika baada ya
miaka miwili.
Jitihada
zote hizo, lengo lake ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya
2015-2020, ambayo inataka hadi ifikapo mwaka 2020, wananchi waliounganishwa na
umeme wafikie asilimia 60 na kiwango cha uzalishaji kifike megawati 4,915.
Mbali na
malengo ya Ilani hiyo, jitihada hizo pia zitachangia katika kutekeleza Dira ya
Maendeleo ya Taifa inayotaka Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025, ambayo imeweka lengo la usambazaji umeme liwe asilimia 50 mwaka huo mwaka
2025 na asilimia 70 mwaka 2033.
Tayari
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameshaelezea nia ya
Serikali kutaka sekta ya nishati itoe mchango mkubwa kufikia uchumi huo wa
kati, kwa kuwa rasilimali za kufikia lengo hilo kupitia nishati zipo na
kinachotakiwa ni dhamira na kasi ya kutekeleza.
Katika
kusisitiza kasi na dhamira hiyo ya Serikali, Waziri huyo amekuwa akielezea
mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa dira hiyo, iliyotaka ifikapo
mwaka 2015 uunganishaji umeme uwe umefikia asilimia 30. Lakini, kutokana na
utekelezaji madhubuti wa dira hiyo, kiwango hicho kilivukwa lengo na kufikia
asilimia 40 mwaka 2015.
JPM
na Marekani
Mbali na msaada huo wa Uingereza katika kusambaza umeme vijijini, Serikali ya Marekani pia imeelezea kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, hatua iliyoanza kuvutia wawekezaji wa nchi hiyo.
Mbali na msaada huo wa Uingereza katika kusambaza umeme vijijini, Serikali ya Marekani pia imeelezea kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, hatua iliyoanza kuvutia wawekezaji wa nchi hiyo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Sarah
Sewall, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu Majaliwa nchini Uingereza katika
mkutano huo wa kimataifa, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika
mapambano dhidi ya rushwa.
Alisisitiza
kuwa kampuni nyingi za Marekani, zimeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania. “Ninaamini
uwekezaji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu.
Tunampongeza Rais Dk Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza
kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo
yetu ya siku zote,” alisema.
Majaliwa
ashukuru
Akizungumza katika kikao chake na Waziri Sewall, Waziri Mkuu Majaliwa alimsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza Wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini.
Akizungumza katika kikao chake na Waziri Sewall, Waziri Mkuu Majaliwa alimsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza Wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini.
Alimhakikishia
kuwa Watanzania wamekuwa wakijifunza teknolojia mpya na za kisasa.
Kuhusu mafanikio katika mapambano na rushwa, Majaliwa alisema mkutano huo wa kimataifa, uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani, ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo.
Kuhusu mafanikio katika mapambano na rushwa, Majaliwa alisema mkutano huo wa kimataifa, uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani, ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo.
Akizungumza
na mawaziri hao, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba viongozi wa Serikali wa
Awamu ya Tano, wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu, linalotokana na janga
la rushwa na wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa
mazoea.
“Sasa
hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi
kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga
vita rushwa, ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongoni mwa watu wetu,” alisema.
Alipoulizwa
nini kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hiyo, Waziri
Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa
isitolewe ama kupokelewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya
sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.
“Serikali
inachukua hatua za kiutawala na kisheria, kama vile kuanzisha Mahakama Maalumu
ya Mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UINGEREZA KUSAIDIA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI.”
Post a Comment