Friday, May 20, 2016
TGNP YALIA NA UDHALILISHAJI WANAWAKE
Do you like this story?
KUTOKANA
na matukio ya udhalilishaji dhidi ya wanawake kuongezeka kwa kasi nchini,
taasisi zinazotetea haki za wanawake na watoto, zimevitaka vyombo vya dola
kuamka na kuchukua hatua za haraka zitakazosaidia kukomesha matukio hayo
Akizungumza
jana na waandishi wa habari Dar es Salaam Lilian Liundi, Mkurugenzi Mtendaji wa
Mtandao wa Jinsia (TGNP), akiwa na wanaharakati wengine alisema kuwa, tangu
Januari hadi kufikia Aprili mwaka huu matukio ya udhalilishaji na unyanyasaji
dhidi ya wanawake yamekuwa yakizidi kushika kasi.
“Tuko
hapa kwa pamoja tukilaani vikali ukatili dhidi ya wanawake unaoendelea
kukithiri nchini, mfano kuna tukio lilitokea hivi karibuni katika mji mdogo wa
Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambapo binti wa miaka 21 alikuwa
akibakwa na picha za video dhidi ya tukio hilo kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii,
“Si
hilo tu bali taarifa tulizozikusanya juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia
tangu mwaka huu uanze ni mengi katika kila kona ya Tanzania, tunaona Aprili
mwaka huu Yunis Peter mkazi wa Dar, alichomwa na kitu chenye ncha kali katika
nyumba ya kulala wageni, Rehema Lubinza mkazi wa Mlele, aliuwawa kikatili kwa
kukatwa na mapanga na mumewe kisha mwili wake kufungiwa ndani, si hivyo bali
tukio la muuguzi wa Zahanati ya Kagu Geita, bi Elizabeth Msango, ambaye
aliuwawa na watu wasiojulikanayapo matukio mengi ambayo ni unyanyasaji
unaonekana kabisa”alisema.
Akizungumzia
kuhusu udhalilishaji uliofanywa Mvomero, Gladness Munuo, Mratibu wa dawati la
usuluhishi kutoka chama cha Wahariri Wanawake Tanzania, (TAMWA), alisema tukio
hilo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura 16(Kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 ambayo imeainisha makosa ya kujamiana).
Alisema
pamoja na sheria za ndani, serikali ya Tanzania imeridhia mikataba na matamko
mengi kuhusu haki za wanawake na usawa wa kijinsia ikiwamo mkataba wa
kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake(CEDAW), pamoja na mkataba wa
haki za watoto (CRC), sambamba na tamko la kimataifa la haki za binadamu
(UDHR,19),ambalo linatambua haki za wanawake na watoto.
Theodosia
Nshala, Mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake (WLAC), alisema
kama kituo tayari wameshapokea kesi kumi na mbili lakini licha ya kufanya
jitihada za kuzishughulikia bado wahusika ama waathirika wamekuwa wakikata
tamaa kutokana na kesi hizo kuchukua muda mrefu ambapo kesi moja ambayo ina
ushahidi uliojitosheleza inaweza kuchukua hata miaka mitatu mpaka mitano .
Grace
Mwangamila, Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na haki za binadamu(LHRC),
alisema kupitia tafiti zao matukio ya udhalilishaji dhidi ya wanawake yameoneka
kuwa mengi huku kwa upande wa watoto udhalilishaji na unyanyasaji umebainika
ukifanyika ndani ya familia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TGNP YALIA NA UDHALILISHAJI WANAWAKE ”
Post a Comment