Thursday, May 19, 2016
HAWA NDIO WAREMBO 11 WATAKAO WANIA TAJI LA MISS MBEYA KESHO.
Do you like this story?
WAREMBO 11 wanatarajia
kupanda Jukwaani ijumaa hii(Mei 20) kuwania taji la Miss Mbeya 2016 kwenye
mashindano yatakayofanyika katika Hotel ya Paradise,Soweto jijini Mbeya.
Warembo wanaowania taji
hilo ni Emmiliana Abdalla,Anitha Patric,Aziza Lysamuya,Praxeda Geofray,Juliana
Gilbert,Nancy Matta,Agnes Boliva,Julitha Mponela,Afrodisia Chapa,Eunicer
Robert,Priscar Mengi na Juliana Lyampawe.
Mratibu wa mashindano
hayo Tom Chilala amesema maandalizi yote yamekamilika na kilichobakia ni
warembo kupanda jukwaani mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala atakayekuwa
mgeni rasmi.
Chilala amesema kuwa
majaji wa shindano hilo akiwemo mwenyekiti wa shindano la Miss Kanda ya nyanda
za juu kusini Dosi Magambo ndiyo watakaosimamia vigezo vyote vya kuchagua
mshindi.
“Shindano linatarajiwa
kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na muonekano wa warembo wa mwaka huu
na pia umaarufu alionao kwa sasa msanii Hamornize atakayepamba onesho hili”
“Awali washiriki walikuwa
kumi na tano lakini baada ya kuwachuja wakiwa kambini wamebakia kumi na moja
ambao ndiyo watapanda jukwaani kuwania taji”anasema Chilala.
Mratibu huyo amesema
mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atazawadiwa fedha taslimu shilingi
laki saba,wa pili laki nne,wa tatu laki tatu na wan ne laki mbili huku
waliosalia wakipewa kifuta jasho cha shilingi 80,000 kila mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAWA NDIO WAREMBO 11 WATAKAO WANIA TAJI LA MISS MBEYA KESHO.”
Post a Comment