Saturday, June 25, 2016
HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA HUENDA IKASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UTENGENEZAJI MADAWATI.
Do you like this story?
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mch David Mwashilindi akimkabidhi Mmoja wa walimu waSule za Sekondari Madawati. |
Baadhi ya Walimu akisubiria kukabidhiwa Madawati yao ambayo yameisha kamilika. |
Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Mch David Mwashilindi akimkabidhi Mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Madawati. |
Halmashauri
ya jiji la Mbeya huenda ikashindwa kutekeleza agizo la Rais John Pombe
Magufuri, lililozitaka halmashauri kuhakikisha zinamaliza tatizo la uhaba
wa madawati shuleni ifikapo Juni 31, mwaka huu kutokanana kutokuwepo kwa
msukumo wa kutosha katika utekelezaji wa agizo hilo.
Halmashauri
ya Jiji la Mbeya, imeweza kutengeneza na kukamilisha madawati 1500, wakati
uhitaji ni madawati 10,000.
Katika
upungufu huo, shule za msingi zinauhitaji wa madawati 9894, wakati sekondari
zikihitaji madawati 605.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa utengenezaji wa madawati
katika chuo cha ufundi VETA jijini Mbeya , Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mussa
Mapunda, alisema katika madawati hayo 1500 ambayo tayari yamekamilika, madawati
798 ni ya shule za msingi huku madawati 477.
Alisema,
kupatikana kwa madawati hayo 477 kwa shule za sekondari halmashauri itakuwa
imemaliza deni kwa upande huo na kubaki na deni la madwati 9096 kwa shule za
msingi ambao nayo yapo katika mchakato wa kukamilika.
Akizungumza
na baadhi ya wananchi wakiwemo wanafunzi, madiwani na watumishi wa serikali,
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, alisema madawati 9096 ambayo
yanahitajika katika shule za msingi yapo katika mchakato wa kukamilika.
Aidha,
Meya huyo alisema, licha ya halmashauri hiyo kukabiliwa na changamoto ya
rasilimali fedha lakini imeweza kufanya kazi hiyo kwa haraka hasa ukiangali ni
kipindi kifupi tu, tangu kuungua moto kwa mabweni zaidi ya mawili ya shule ya
sekondari ya iyunga na kuteketeza vitanda 150 na magodoro yake.
“Ninawashukuru
wadau kwa kujitolea kwani wakati wakichangia shule ya Iyunga, suala la madawati
nalo likaingia hivyo ninaamini kwamba halmashauri itaweza kukamilisha tatizo la
madawati na wanafunzi wote kuondokana na tatizo la kukaa chini,”alisema.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA HUENDA IKASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UTENGENEZAJI MADAWATI.”
Post a Comment