Friday, June 24, 2016

RAIS KAGAME KUWA MGENI RASMI KWENYE MAONESHO YA SABASABA



Rais wa  Rwanda Paul Kagame, anatarajiwa kuzindua Maonesho ya Wafanyabishara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba ambayo hufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi  Agustino Mahiga amesema Rais Kagame ambaye ndiye mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Sabasaba anatarajiwa kuwawasili nchini Julai Mosi mwaka huu.

“Ujio wa Rais huyu kutoka nchini Rwanda umekuja baada ya Rais wa Awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuomba kuja kutembelea Tanzania ili kuweza kudumisha ushirikiano wa kikanda wa wa nchi hizi mbili katika Jumuia ya Afrika Mashariki” Alisema  Mahiga .
 


0 Responses to “RAIS KAGAME KUWA MGENI RASMI KWENYE MAONESHO YA SABASABA ”

Post a Comment

More to Read